JINSI YA KUFUNGA SOLAR PANEL

Baada ya kuangalia aina za solar panel na kazi zake katika makala ziliyopita kama hujazisoma bofya hapa leo tunaangali jinsi ya kufunga solar panel ili kuweza kupata umeme wa kutosaha katika kipindi chote cha mwaka. Fuatana nami ndugu msomaji mzuri makala hii.

1. VIFAA

 • nyundo
 • misumali
 • mbao nzuri
 • panel yako
 • angle measure
 • multimeter
 • wire
2. VITU VYA KUJUA KABLA YA KUANZA KUFUNGA PANEL YAKO
 1. kujua mwelekeo wa paa lako na jinsi lilivyo
 2. Hali ya hewa ya eneo husuka
 3. kujua upo kwenye hemisphere gani
 4. kujua upo kwenye latitude gani
3.HATUA ZA KUFUATA UNAPOANZA KUFUNGA SOLAR PANEL YAKO
kwanza kabisa najua unajiuliza kuwa nawezaje kuifanya panel yangu iweze kuzalisha umeme wa kutosaha ktika kipindi chote cha mwaka mzima bila matitizo yoyote, ondoa shaka hapa nitaelezea kwa undani zaidi jinsi unavyoweza kufanikiwa kwa hili fuatana nami vizuri kama utakuwa sehemu hujaelewa unaruhusiwa kuuliza ebu tuanza:
 1. KUJUA MWELEKEO WA PANEL YAKO
Kwanza kabisa unapodesign panel yako unatakiwa kuamua panel yako unaifunga kwenye paa gani ambalo hua linapokea kiwango kikubwa cha jua muda mwingi na angle gani kwa ajili ya kupata umeme wa kutosha. Kwa sababu ili kupata umeme wa kutosha panel yako inatakiwa iwe perpendicular na miale ya mwanga. Mwelekeo mzuli ambao tunashauliwa ni kuelekea south (azmuth angle =0)
Kama ikitokea upande wa kusini kuna kivuli cha miti au majengo unaweza ukavary angle ili kuweza kupata kiwango kikubwa cha umeme.
    2. KUJUA KIWANGO CHA ANGLE CHA KUSET
Tayari tumeshajua kuwa mwelekeo mzuri ni kusini (south) kinachofuata ni kujua angle ngapi inatakiwa ili kuweza kuzalisha umeme kwa wingi najua ndo shauku yetu ya kutaka kujua fuatana nami msomaji wa makala hii.
Tukijua kuwa tayari mapaa ya nyumba zetu yapo katika angle fulani ni vizuri ukaifahamu ili ikusaidie kupata maximum angle. Lakini kama unaitaji kuweka panel yako katika eneo la wazi hii makala itakusaidia kupata angle nzuri.
Kupata maximum anlge kunategema na vitu viwili
 • Latitude ya eneo husika ulilopo
 • Na muda ambao unaitaji upate nishate hiyo kwa mwaka
The angle ya kufunga paneli yako ni sawa na stations latitude jumlisha na 15 kipindi cha winter na station latitude toa 15 kipindi cha summer. Hii inaongeza uzalishaji wa panel yako.

Lakini kutokana na kubadilika badilika kwa kiwango cha jua mwezi hadi mwezi unaweza ukafunga standi kama wanazofunga kwenye dish satellite yaani ungo kama wa azam ili uweze kuadjust kila mwezi kwa kutumia anle calculator hii hapa  ambapo hizo ange zipo kutoka vertical kwa hiyo itakusaidia ukiitaji kufunga huo mfumo.

3. JINSI YA KUFUNGA PANEL YAKO SASA

Hapa tunaona baada kuwa tayari na vifaa vyako vyote vya ufundi na tayari umeshapima angle ya paa lako wakati tayari unajua tilth angle ( The angle ya kufunga paneli yako ni sawa na stations latitude jumlisha na 15 kipindi cha winter na station latitude toa 15 kipindi cha summer). Na kama unaitaji kuweka sola panel yako katika eneo la wazi na sio paa kuna vifaa unatkiwa kuwa navyo kama pole inaweza kuwa ya chuma au hata zege au concrete beam.

Kinachofuata ni upimaji wa izo angle huku ukizingatia direction ya panel inatakiwa kuwa perpendicula na jua yaan south.

 • Pima angle ya paa lako kwa kutumia njia yoyote kutoka horizontal
 • kama angle ya paa inakalibiana kwa kiwango kidogo na tilt angle yako solar panel yako inatakiwa uiweke juu yaa paa lako na kama tilt angle ni kubwa kuliko paa angle lazima utengeneze stand ambayo itafidia kiasi cha angle kilichobaki kufikia tilt angle.
 • Baada ya kila kitu kuwa sawa pamoja na uelekeo kuwa kusini yaan perpendicular na jua ufungaji unaendelea kwa mtu ambaye ana ujuzi kidogo na ufundi selemala yaan caperter.
 • Kama utatumia mbao unatakiwa uzilinde na dawa maalimu ya kuzuia wadudu waharibifu kwa sababu itaweza patwa na mvua na kazalika kama utatumia steel sawa.
 • kama utaitaji kuunganisha panel zako katika series au pararel kutokana na matumizi yako unaweza lakini vitu vya kuzingatia ni mwelekeo wa panel zako na tilt angle baasi.
BAADA YA LEO KUANGALIA JINSI YA KUFUNGA SOLAR PANEL KIFUATACHO TUTAONA JINSI YA KUANGANISHA VIFAA VILIVYOBAKI KAMA BATTERY.INVERTOR, CHARGE CONTROLLER NA WIRE RING KWA UJUMLA.
TAHADHARI:KUUNGANISHA UMEME WA KUTOKA KATIKA PANEL YAKO IWE HATUA YA MWISHO KABISA BAADA YA KUKAMILISHA WIRE RING YAKO .

LEAVE REPLY

Your email address will not be published. Required fields are marked *